• HABARI MPYA

    Thursday, July 07, 2022

    DOGO WA YANGA B APIGA HAT-TRICK MICHUANO YA U20


    MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Clement Francis Mziza amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick kwenye Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20.
    Nyota huyo alifunga mabao yote matatu akiisaidia timu yake kushinda 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Mechi nyingine ya Kundi D jana, KMC ilitoa sare y 1-1 na Kagera Sugar, wakati Kundi B, Mbeya Kwanza iliichapa 3-1 Ruvu Shooting na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wakaitandika 4-0 Dodoma Jiji.
    Michuano hiyo ilianza juzi, Kundi A; Biashara United ikitoka sare ya 0-0 na Namungo FC na Simba SC ikaichapa Polisi Tanzania 2-1, wakati Kundi C, Tanzania Prisons iliichapa Coastal Union 1-0 na wenyeji, Azam FC wakaichapa Mbeya City 3-2.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DOGO WA YANGA B APIGA HAT-TRICK MICHUANO YA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top