• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2022

  PRISONS YAICHAPA JKT 1-0 MBWENI MCHUJO KUBAKI LIGI KUU


  TIMU ya Tanznaia Prisons imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Oscar Paul dakika ya 38, sasa timu hizo marudiano Jumatano Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao, wakati atakayefungwa atacheza Championship.
  Ikumbukwe Prisons imeingia kwenye mechi hii ya mchujo wa kuwania kucheza Ligi Kuu baada ya kutolewa na Mtibwa Sugar katika mchujo wa awali uliohusisha timu za Ligi Kuu, wakati JKT imetoka Championship.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA JKT 1-0 MBWENI MCHUJO KUBAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top