• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 12, 2020

  RONALDO AFUNGA URENO YASHINDA 7-0 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI


  Cristiano Ronaldo (kushoto) akishangilia na Diogo Jota baada ya kuifungia Ureno bao la sita dakika ya 85 katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Andorra kwenye mchezo wa kirafiki usiku wa jana Uwanja wa Luz, Lisbon kwenye mchezo wa kirafiki. Ronaldo mwenye umri wa miaka 35, amefikisha mabao 102, sasa akizidiwa saba na Ali Daei wa Iran katika anayeongoza kufunga mabao mengi kwenye mechi za kimataifa. Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Pedro Neto dakika ya nane, Paulinho dakika ya 29 na 61, Renato Sanches dakika ya 56, Emili Garcia aliyejifunga dakika ya 76 na Joao Felix dakika ya 88
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA URENO YASHINDA 7-0 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top