• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 30, 2020

  NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN KUSINI 1-0, KUMENYANA NA UGANDA FAINALI CECAFA U-20


  TANZANIA imefanikiwa kwenda Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini jioni ya leo Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mkoani Arusha.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee la Tanzania Kassim Haruna dakika ya 56 na sasa Ngorongoro Heroes itamenyana na Uganda katika fainali iliyoitoa Kenya.
  Katika Nusu Fainali ya kwanza, The Kobs waliichapa Kenya 3-1 hapo hapo Uwanja wa Black Rhino Academy na watamenyana na Tanzania Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN KUSINI 1-0, KUMENYANA NA UGANDA FAINALI CECAFA U-20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top