• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 30, 2020

  AZAM FC YATANGULIA KIPINDI CHA KWANZA, BIASHARA UNITED WACHOMOA KIPINDI CHA PILI, 1-1

  AZAM FC imetoa sare ya 1-1 na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume Musoma mkoani Mara.
  Ayoub Lyanga alianza kuifungia Azam FC dakika ya 20, lakini Timothy Omwenga akaisawazishia Biashara United dakika ya 59.
  Azam FC iliyokuwa inacheza mechi ya kwanza baada ya kumfukuza kocha wake Mromania, Aristica Cioaba, inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 13 na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikizidiwa pointi tano na vinara, Yanga SC.
  Biashara United yenyewe inafikisha pointi 19 baada ya mechi 13 pia na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, ikiizidi KMC pointi moja, ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YATANGULIA KIPINDI CHA KWANZA, BIASHARA UNITED WACHOMOA KIPINDI CHA PILI, 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top