• HABARI MPYA

    Wednesday, November 25, 2020

    TFF YAKANA KUPOKEA MGAWO WA RAIS WA CAF ALIYEFUNGIWA KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA

     

    SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF), limesema hakuna fedha kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad iliyoingizwa kwenye akaunti binafsi ya Rais wa TFF, Wallace Karia.
    Utetezo huo unafuatia Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kumfungia Rais wa CAF, Ahmad kujihusisha na shughuli za soka kwa miaka mitano pamoja na kutozwa faini ya dola za Kimarekani 200,000 kwa tuhuma na ukiukaji sheria na maadili ya Kiofisi.
    Na CAF imemteua aliyekuwa Makamu wake, Constant Selemani Omari kuwa kaimu Rais wa Shirikisho hilo la Soka barani kuelekea uchaguzi Mkuu Machi mwakani.
    Makamu huyo wa rais wa FIFA mwenye umri wa miaka 60 amedaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na utumizi mbaya wa fedha.
    Uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Mecca ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine , ilisema taarifa ya FIFA.
    Mwezi uliopita makamu, Ahmad raia wa Madagascar alitangaza lengo lake kuwania muhula wa pili wakati uchaguzi wa CAF utakapofanyika Machi mwakani.
    Hilo huenda lisifanyike kwa sababu atalazimika kupita mtihani wa maadili ili kustahiki kusalia katika baraza la Fifa.
    Uwezekano wa yeye kuchaguliwa ka awamu ya pili utategemea iwapo atashinda kesi ya rufaa aliowasilisha katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS), huku kesi hiyo akihakikisha kuwa inasikilizwa mapema ili kumruhusu kuthibitishwa kuwa mgombea.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAKANA KUPOKEA MGAWO WA RAIS WA CAF ALIYEFUNGIWA KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top