• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 26, 2020

  PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU BAADA YA KUUMIA DHIDI YA YANGA JANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mzimbabwe wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo, aliyeumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam anatarajiwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
  Taarifa ya Azam FC leo imesema kwamba Dube mwenye umri wa miaka 23, aliumia dakika ya 15 kwa kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wake wa kushoto uitwao Ulnar, unaoanzia kwenye kiwiko na kushuka hadi kwenye kidole cha mwisho.
  Taarifa hiyo imesema kwamba Dube ataondoka nchini Jumapili ya Novemba 29 kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways (KQ) na atatibiwa kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo Cape Town, chini ya daktari bingwa wa mifupa, Robert Nicolas.


  Tangu mwaka 2011 Azam FC imekuwa ikiitumia hospitali hiyo kuwatibia wachezaji wake kwa mafanikio na wengi wamekuwa wakipona vizuri na kurejea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRINCE DUBE KUPELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU BAADA YA KUUMIA DHIDI YA YANGA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top