• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 26, 2020

  NGORONGORO HEROES YAITANDIKA SOMALIA 8-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI CECAFA U-20 KIBABE

  Wachezaji wa Tanzania wakipongezana kwa ushindi wa 8-1 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa Kundi A michuano ya CECAFA U20 leo Uwanja wa Black Rhino Academy uliopo Karatu mkoani Arusha. Mabao ya Ngorongoro Heroes yamefungwa na Hamisi Suleiman dakika ya tatu, Ben Starkie dakika ya 14, Kelvin John 'Mbappe' dakika ya 28, 33 na 55, KassimHaruna dakika ya 47, Frank George dakika ya 65 na Anuary Jabir dakika ya 86, wakati la Somalia limefungwa na Sahal Muhumed dakika ya sita.
  Kwa ushindi huo, Tanzania inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo 'Julio' inafikisha pointi sita na kuongoza Kundi A ikitinga Nusu Fainali ambako itakutana na Mshindi wa Pili Bora baina ya makundi yote Jumatatu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAITANDIKA SOMALIA 8-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI CECAFA U-20 KIBABE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top