• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 29, 2020

  MLANDEGE YACHAPWA 5-0 NA CS SFAXIEN YA TUNISIA PALE PALE ZANZIBAR LIGI YA MABINGWA

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  TIMU ya Mlandege FC ya Zanzibar imeanza vibaya michuano ya Afrika, baada ya kuchapwa 5-0 na CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezi wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa jana uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Baada ya kipigo hicho, sasa Mlandege itatakiwa kwenda kushinda kuanzia 6-0 kwenye mchezo wa marudiano Tunisia ili kusonga mbele Ligi ya Mabingwa.
  Mshambuliaji Mnigriaa Eduwo Kingsley alifunga bao la kwanza dakika ya 30, kabla ya Watunisia, beki Hani Amamou kufunga la pili dakika ya 41 na mshambuliaji Firas Chaouat kufunga matatu mfululizo dakika ya 56, 78 na 84.


  Juzi, Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, KVZ walichapwa 1-0 na Alamal Atbara, bao pekee la Captain Basheer dakika ya 12, Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman, Sudan.
  Tanzania Bara, Namungo FC wao walianza vyema Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji Dar es Salaam.
  Mabao ya Namungo FC katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali yamefungwa ma Mghana Steven Sey dakika ya 20 na 39 na Shiza Kichuya dakika ya 64 na timu hizo zitarudiana wiki ijayo Sudan Kusini.
  Leo ni zamu ya wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC ambao watamenyana na wenyeji, Plateau United kuanzia Saa 10:00 jioni kwa Saa za Afrika Magharibi na Saa 12:00 kwa Saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Jos katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MLANDEGE YACHAPWA 5-0 NA CS SFAXIEN YA TUNISIA PALE PALE ZANZIBAR LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top