• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 20, 2020

  RUVU SHOOTING YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 UHURU, PRISONS YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA MTIBWA SUMBAWANGA

  Na MwandIshi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABAO ya William Patrick dakika ya 12, Abraham Mussa dakika ya 53 na Fully Zulu Maganga dakika ya 90 na ushei yameipa Ruvu Shooting ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Nayo Dodoma Jiji FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

   
  Biashara United ilitangulia kwa bao la Lenny Kissu dakika ya 62, kabla ya mkongwe Khamis Mcha kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 78, wote wakifunga kwa mikwaju ya penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 UHURU, PRISONS YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA MTIBWA SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top