• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 14, 2020

  TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 TUNISIA NA KUJIWEKA PAGUMU MBIO ZA AFCON YA 2021 CAMEROON

  Na Mwandishi Wetu, TUNISIA
  TANZANIA imejiweka kwenye nafasi ngumu katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Tunisia katika mchezo wa Kundi J usiku wa jana Uwanja wa Uwanja wa Hamadi Agrebi Olimpiki mjini Rades.
  Bao pekee lililoizamisha Taifa Stars lilifungwa na Nahodha wa Carthage Eagles , Youssef Msakni anayechezea klabu ya Al-Duhail ya Qatari kwa penalti dakika ya 14  baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na kipa wa Tanzania, Aishi Salum Manula kwenye boksi.
  Carthage Eagles waliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini wakashindwa kupata mabao zaidi kutokana na wageni kucheza kwa kujilinda.


  Hicho kinakuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Tanzania chini ya Kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragije baada ya kuchapwa 2-1 na Libya hapo hapo Tunisia mechi ya Kufuzu AFCON pia na 1-0 na Burundi katika mchezo wa kirafiki Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Tanzania inaendelea kushika mkia Kundi J ikibaki na pointi zake tatu sawa na Libya na Equatorial Guinea, wakati Tunisia itahitaji pointi tatu zaidi katika mchezo wa marudiano na Taifa Stars Dar es Salaam siku tatu zijazo ili kutia kibindoni tiketi ya Cameroon mwakani.
  Kikosi cha Tunisia kilikuwa; Farouk Ben Mustapha, Mohamed Drager, Dylan Bronn, Yassine Meriah, Ali Maaloul, Anis Ben Slimane/ Naim Sliti dk71, Ellyes Skhiri, Ferjani Sassi/ Marc Martin Lamti dk90, Hamza Rafia/ Ayman Ben Mohamed dk88, Wahbi Khazri/ Nabil Makni dk90 na Youssef Msakni/ Saif-Eddine Khaoui dk71.
  Tanzania; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Bakari Mwamnyeto/Feisal Salum dk80, Jonas Mkude, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Simon Msuva/Ditram Nchimbi dk85 na Farid Mussa/Iddi Nado dk61.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 TUNISIA NA KUJIWEKA PAGUMU MBIO ZA AFCON YA 2021 CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top