• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 29, 2020

  SIMBA SC YAWAZIMA WANIGERIA KWAO, YAWACHAPA PLATEAU UNITED 1-0 MFUNGAJI CHAMA JOS

  Na Mwandishi Wetu, JOS
  SIMBA SC imetanguliza mguu mmoja mbele Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Plateau United jioni ya leo Uwanja wa Kimataifa wa Jos International, Jijini Jos nchini Nigeria
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzambia Clatous Chota Chama dakija ya 53 akimalizia kazi nzuri ya winga kutoka Msumbiji, Luis Jose Miquissone.
  Sasa mabingwa wa Tanzania watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumamosi ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Wakifanikiwa kuitoa Plateau United, SImba SC watakutana na mshindi kati ya Costa do Sol ya Msumbiji na Platinum FC ya Zimbabwe kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.
  Mechi ya kwanza jana, Platinum FC walishinda 2-1 ugenini Uwanja wa Taifa wa Zimpeto Jijini Maputo, Msumbiji na timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare, Zimbabwe. 
  Kikosi cha Plateau United kilikuwa; Adamu Abubakar, Ibrahim Babawo, Dennis Nya, Andrew Ikefe, Gabriel Wassa, Isah Ndala, Oche Ochewechi, Sunday Adetunji, Abba Umar, Uche Onuasonya/Sunday Anthony dk63 na Saeed Jibrin/Benard Ovoke dk46.
  Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango/Muzamil Yassin dk46, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/Berrnard Morrison dk78, Erasto Nyoni, John Bocco, Clatous Chama/Ibrahim Amedk90 na Luis Miquissone.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWAZIMA WANIGERIA KWAO, YAWACHAPA PLATEAU UNITED 1-0 MFUNGAJI CHAMA JOS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top