• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 25, 2020

  COASTAL UNION YAZINDUKA NA KUICHAPA IHEFU SC 1-0 MKWAKWANI, MBEYA CITY NAO WASHINDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la Salum Ally dakika ya 16 limetosha kuipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Ushindi unaofuatia kipigo cha 7-0 kutoka kwa mabingwa watetezi, Simba SC kinaifanya Coastal Union ifikishe pointi 15 baada ya kucheza mechi 12 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya 10.
  Uwanja wa Chuo cha Ushirika, bao pekee la beki Pato Ngonyani dakika ya pili likaipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.


  Naye Kibu Dennis akaibuka shukaa wa Mbeya City baada ya kufunga bao pekee dakika ya 68 katika ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAZINDUKA NA KUICHAPA IHEFU SC 1-0 MKWAKWANI, MBEYA CITY NAO WASHINDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top