• HABARI MPYA

    Tuesday, November 10, 2020

    MWAKINYO ATAMBA KUMDUNDA MUARGENTINA HADI ASTAAFU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BONDIA Hassan Mwakinyo ameahidi kumpiga mpinzani wake, Muargentina Jose Carlos Paz na kutetea taji lake ubingwa wa Mabara wa WBF uzito wa Super-Welter katika pambano la raundi 12 Ijumaa ukumbi wa Next Door Arena, Masaki Jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo hoteli ya Colosseum, Masaki, Mwakinyo amesema kwamba atahakikisha Paz anaachana na mchezo wa ngumi za kulipwa kutokanana kipigo alichumuandalia.
    “Natamani pambano lifanyike mapema iwezekanavyo, hata siku moja kabla kwani nipo fiti zaidi ya nilivyokuwa mwanzoni. Sitaki kuwanyong’onyesha Watanzania katika pambano hilo,” alisema Mwakinyo.


    Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa akiwatambulisha Hassan Mwakinyo na Jose Carlos Paz leo hoteli ya Colosseum, Masaki 

    Alisema kuwa anajua kuwa Paz ni bondia mzuri na amejiandaa vyema katika pambano hilo, lakini kutokana na jinsi alivyojiandaa, hatakuwa na nafasi ya kutamba kwake.
    Kwa upande wake, Paz alisema kuwa hakuja nchini kutembea zaidi ya kuwania ubingwa wa ambao Mwakinyo anao.
    “Nipo vizuri, mazoezi yangu nchini yamekuwa na mafanikio makubwa na hali ya hewa siyo tatizo. Nitamfundisha ngumi Mwakinyo ,” alisema Paz.
    Kwa mabondia hao kutambiana pia bondia Hussein Itaba na mpinzani wake kutoka DR Congo, Alex Kabangu, Fatuma Zarika dhidi ya  Patience Mastara (Zimbabwe) na Mtanzania Zulfa Macho ambaye atazichapa na Alice Mbewe wa Zambia  pia walitambiana.
    Mkurugenzi wa Jackson Group Sports, Kelvin Twissa alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kuwaomba mashabiki kuendelea kununua tiketi kwa ajili ya pambano hilo.
    “Maandalizi yapo vizuri na kama mnavyoona mabondia wote wapo hapa na sas tunamsubiri  Rais wa WBF, Howard Goldberg na mwamuzi Edward John Marshall ambao watawasili leo Jumatano Novemba 11,” alisema Twisa.
    Twissa alisema tiketi zitaanza kuuzwa kwa njia ya Nilipe na Selcom kwa Sh 3 Milioni kwa meza ya watu 10 na  Sh150,000 kwa kwa viti vya kawaida.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAKINYO ATAMBA KUMDUNDA MUARGENTINA HADI ASTAAFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top