• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 20, 2020

  YANGA SC YAMTEUA HAJI MFIKIRWA KUWA KAIMU KATIBU MKUU MPYA BAADA YA KUMSIMAMISHA PATRICK

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Yanga SC umemteua Mkurugenzi wake wa Fedha, CPA Haji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu, akichukua nafasi ya Wakili Simon Patrick aliyesimamishwa.
  Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwakalebela amesema Mfikirwa atashika wadhifa huo hadi hapo uongozi utakapoteua mtu mwingine kushika nafasi hiyo.
  Kwa upande wake, Mfikirwa amesema kikubwa kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha anasimamia na kufanikisha mipango yote ya klabu ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Mengine ni mabadiliko ya uendeshaji wa klabu na ujenzi wa hostel na Uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo Kigamboni.


  Katika hatua nyingine, Yanga imeliomba Shirikisho la Tanzania (TFF) kusikiliza kesi yao dhidi ya mkataba wa Bernard Morrison na Simba kabla ya dirisha dogo la usajili halijafunguliwa Dec 15 mwaka huu.
  Yanga waliwasilisha malalamiko yao kwa TFF wakidai kuwa mkataba uliyopo kwenye system kati ya Mchezaji huyo na waajiri wake Simba ni batili kwa kuwa haujasainiwa na Kiongozi yoyote wa Simba.
  Mwakalebela anasema, hofu yao ni kwamba kipindi cha dirisha dogo mkataba huo unaweza kubadilishwa kwa sababu system inakuwa ipo wazi kwa sababu Mchezaji huyo amewasilisha mkataba ambao umesainiwa na pande zote katika Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS kitu ambacho kimewashangaza. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTEUA HAJI MFIKIRWA KUWA KAIMU KATIBU MKUU MPYA BAADA YA KUMSIMAMISHA PATRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top