• HABARI MPYA

  Sunday, November 29, 2020

  POLISI TZ YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA COASTAL UNION MOSHI, PRISONS YAICHAPA MWADUI FC 2-0 SUMBAWANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar e Salaam.
  Tariq Seif Kiakala alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 50, kabla ya Raizin Hafidh kuisawazishia Coastal Union dakika ya 75. 
  Polisi Tanzania inafikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 13, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa pointi tatu na zote, Ruvu Shooting na Simba SC zinazofuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Coastal Union inafikisha pointi 16 baada ya mechi 13 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting ya Pwani imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Ruvu Shooting imefikisha pointi 23 baada ya mechi 13 pia na kuendelea kukamata nafasi ya nne, nyuma ya Simba SC yenye pointi 23 za mechi 11.
  Katika mchezo uliotangulia mchana, Tanzania Prisons iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa mabao ya Lambert Sibiyanka dakika ya 23 na Gasper Mwaipasi dakika ya 87.
  Tanzania Prisons imefikisha pointi 19 baada ya mechi 13 na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya tisa, wakati Mwadui FC inayobaki na pointi zake 10 za mechi 13 inaendelea kushika nafasi ya 17 kwenye Ligi Kuu ya timu 18, ikiizidi pointi nne Ihefu SC inayoshika mkia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TZ YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA COASTAL UNION MOSHI, PRISONS YAICHAPA MWADUI FC 2-0 SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top