• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2023

  HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YASHINDA 4-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's, Southampton, Hampshire.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mnorway Erling Haaland mawili dakika za 45 na 68, Jack Grealish dakika ya 58 na Julian Alvarez dakika ya 75 kwa penalti,wakati la Southampton limefungwa na Sékou Mara dakika ya 72.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 67, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 29, wakati Southampton wanaendelea kushika mkia na pointi zao 23 za mechi 30. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YASHINDA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top