• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2023

  KIUNGO WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA MORO


  KIUNGO wa zamani wa timu ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Amri Ibrahim Luchangatira amefariki dunia jana nyumbani kwake Saba Saba mkoani Morogoro baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda. 
  Taarifa zinasema Amri Ibrahim aliyechezea pia klabu za Pamba ya Mwanza, Nyota Afrika ya Morogoro, Mara Spurs, Gungu Rangers na RTC Kigoma pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars anatarajiwa kuzikwa leo Morogoro.
  Amri Ibrahim aliyezaliwa mwaka 1956, pamoja na kucheza Simba kuanzia mwaka 1980 hadi 1986, pia amewahi kuwa kocha wa timu hiyo miaka ya 2000.
  Amri Ibrahim ambaye amewahi kufundisha pia Rhino na Saba Saba United za Morogoro, hadi umauti unamfika alikuwa mmoja wa makocha wa kituo cha kukuza vipaji cha Uluguru Mountains Sports Center ya Morogoro pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA MORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top