• HABARI MPYA

  Saturday, April 08, 2023

  FOUNTAIN GATE WATWAA UBINGWA MICHUANO YA CAF


  TIMU ya Fountain Gate ya Dodoma imetwaa ubingwa wa michuano ya shule za sekondari Afrika kwa wasichana baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco leo Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Katika michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Winfrida Hubert mawili na Irene Chitanda moja na huo ulikuwa mchezo wa pili leo baada awali kuitandika SCG De Mfilou ya Kongo mabao 4-0 katika Nusu Fainali.
  Kwa kutwaa ubingwa huo, Fountain Fate imezawadiwa dola za Kimarekani 300,000, kiasi ambacho pia amepewa bingwa wa upande wa wavulana, huku washindi wa pili wakiondoka na dola 200,000 na wa tatu dola 150,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FOUNTAIN GATE WATWAA UBINGWA MICHUANO YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top