• HABARI MPYA

    Saturday, April 08, 2023

    SEKONDARI YA GUINEA BINGWA KWA WAVULANA MICHUANO YA CAF



    TIMU ya Scolaire Ben Sekou Sylla ya Guinea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya shule za sekondari Afrika kwa wavulana baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 na wenyeji, Clapham High School Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
    Upande wa wasichana Fountain Gate ya Tanzania ndio imekuwa bingwa wa michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya SCG De Mfilou ya Kongo.
    Salima Secondary School ya Malawi imefanikiwa kushika nafasi ya tatu kwa wavulana baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya CEG Sainte Rita ya Benin.
    Kwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, kila timu imezawadiwa dola za Kimarekani 300,000, huku washindi wa pili wakipata dola 200,000 na wa tatu dola 150,000.
    Mchezaji Bora ni Kagiso Maloka wa Clapham High School kwa wavulana na mabingwa, CS Ben Sekou Sylla wametos Kipa Bora Ibrahima Camara wa na mfungaji Bora Mohamed Sacko aliyefunga mabao sita akimzidi moja mchezaji mwenzake wa timu hiyo ya Guinea, Amara Keita.
    Kwa wasichana Mchezaji Bora ni Wilifrida Gerald wa Fountain Gate ambaye pia ameibuka Mfungaji Bora kwa mabao yake 11, huku Kipa Bora ikienda pia kwa Allic Neckema wa Fountain Gate na tuzo ya Mchezo wa Kiungwana imechukuliwa na Anse Boileau wa Shelisheli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SEKONDARI YA GUINEA BINGWA KWA WAVULANA MICHUANO YA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top