• HABARI MPYA

  Saturday, September 03, 2022

  TWIGA STARS YAANZA VYEMA KOMBE LA COSAFA


  MABINGWA watetezi, Tanzania wameanza vyema michuano ya COSAFA kwa wanawake baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Comoro leo Uwanja wa Madibaz mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
  Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na Donisia Minja dakika ya 13 na Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ mawili dakika ya 41 na 52.
  Baada ya mechi hiyo, nyota wa Twiga Stars 
  Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ alipewa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa soka nzuri aliyoonyesha huku akitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa timu yake kutokana na kufunga mara mbili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YAANZA VYEMA KOMBE LA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top