• HABARI MPYA

  Thursday, September 29, 2022

  RUVU SHOOTING YAIBAMIZA COASTAL UNION 2-1 DAR


  WENYEJI, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Ruvu Shooting yamefungwa na Rashid Juma yote dakika ya 36 na 60, wakati la Coastal Union limefungwa na Vincent Abubakar dakika ya nane.
  Kwa matokeo hayo, Ruvu Shooting inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya nne, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake nne nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAIBAMIZA COASTAL UNION 2-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top