• HABARI MPYA

  Sunday, September 18, 2022

  JESUS AFUNGA ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 3-0


  MABAO ya William Saliba dakika ya 17, Gabriel Jesus dakika ya 28 na Fabio Vieira dakika ya 49 yameipa Arsenal ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Brentford leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.
  Kwa ushindi huo, The Gunners wanafikisha pointi 18 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England, wakiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi saba, wakati Brentford inabaki na pointi zake tisa za mechi saba pia nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JESUS AFUNGA ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top