• HABARI MPYA

  Sunday, September 18, 2022

  PHIRI APIGA MBILI SIMBA SC YASONGA MBELE AFRIKA


  MABAO ya mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya 29 na 50 yameipa  Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Lilongwe nchini Malawi, Phiri akifunga moja na lingine, Nahodha, John Bocco.
  Sasa vigogo hao wa Tanzania watakutana na Primiero de Agosto ya Angola iliyoitoa Red Arrows ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 ugenini wiki iliyopita na sare ya 1-1 nyumbani leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI APIGA MBILI SIMBA SC YASONGA MBELE AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top