• HABARI MPYA

  Monday, September 26, 2022

  MAYELE APIGA MBILI, YANGA YASHINDA 4-1 KIGAMBONI


  KLABU ya Yanga jana asubuhi imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Eagle Air Force ya Daraja la Nne katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yalifungwa na Wakongo, beki Joyce Lomalisa na mshambuliaji, Fiston Kalala Mayele mawili na lingine beki Mzanzibari, Ibrahim Bacca.
  Bao pekee la Eagle Air Force ya Ubungo, timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) inayofundishwa na kocha Joseph Kanakamfumu, lilifungwa na Kennedy Bago.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA MBILI, YANGA YASHINDA 4-1 KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top