• HABARI MPYA

  Tuesday, September 13, 2022

  YANGA SC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 3-0 DAR


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Wakongo, beki Djuma Shabani kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 33, Fiston Kalala Mayele dakika ya 38 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 10 na kupanda kileleni ikiizidi pointi mbili Azam FC inayofuatia, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake saba baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 3-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top