• HABARI MPYA

  Wednesday, September 07, 2022

  SIMBA SC YATOA SARE, 2-2 NA KMC LIGI KUU DAR


  VIGOGO, Simba SC wamelazimishwa sare ya 2-2 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake wapya, Mzambia Moses Phiri dakika ya tatu na mzawa, Habib Kyombo dakika ya 89, wakati ya KMC yamefungwa na Matheo Anthony dakika ya 47 na George Makang’a dakika ya 57.
  Simba SC inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza ligi kwa wastani wa mabao dhidii ya mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOA SARE, 2-2 NA KMC LIGI KUU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top