• HABARI MPYA

  Tuesday, September 06, 2022

  YANGA SC NA AZAM FC HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MKAPA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yote leo yamefungwa na walinzi, Mghana Daniel Amoah dakika ya 24 na Msenegal, Malickou Ndoye dakika ya 65, wakati ya Yanga yote yamefungwa na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 57 na 76.
  Beki Mkongo, Djuma Shabani alipoteza nafasi ya kufunga dakika ya 69 baada ya mkwaju wake wa penalti kudakwa na kipa Mcomoro,  Ali Ahamada.
  Yanga inafikisha pointi saba baada ya awali kushinda mechi mbili, wakati Azam FC sasa ina pointi tano baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC NA AZAM FC HAKUNA MBABE, SARE 2-2 MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top