• HABARI MPYA

  Wednesday, September 07, 2022

  CHELSEA YAMFUKUZA TUCHEL BAADA YA KIPIGO JANA


  KOCHA Mjerumani, Thomas Tuchel amefukuzwa Chelsea kufuatia kipigo cha 1-0 jana kutoka kwa Dinamo Zagreb kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Mmiliki mpya, Todd Boehly hajapoteza muda kumtimua Mjerumani huyo baada ya mechi saba za msimu mpya na siku 100 za kuwa kazini tangu airithi timu hiyo kutoka kwa Mrusi, Roman Abramovich. 
  Chelsea inashika nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu ya England na tayari wameanza vibaya katika Ligi ya Mabingwa.
  Chelsea imeruhusiwa kuzungumza na kocha wa Brighton, Graham Potter, ambaye ndiye chaguo la kwanza kuwa mbadala wa Touchel, huku pia ikimpigia hesabu Mauricio Pochettino ambaye hana kazi kwa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAMFUKUZA TUCHEL BAADA YA KIPIGO JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top