• HABARI MPYA

  Friday, September 09, 2022

  PRISONS NA MBEYA CITY ZATOA SARE 1-1 SOKOINE

  WENYEJI, Tanzania Prisons wametoa sare ya 1-1 na wapinzani wao wa Jijini, Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mbeya City walitangulia na bao la Hassan Nassor dakika ya saba, kabla ya mkongwe Khamis Mcha  ‘Vialli’ kuisawazishia Prisons dakika ya 89.
  Kwa matokeo hayo, kila inafikisha pointi nne katika mechi tatu kufuatia kushinda moja na kufungwa moja katika mechi zao za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS NA MBEYA CITY ZATOA SARE 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top