• HABARI MPYA

  Monday, September 26, 2022

  TANZANIA YAITOA SUDAN KUSINI KWA MABAO YA UGENINI AFCON U23


  TANZANIA imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 licha ya sare ya 3-3 na Sudan Kusini leo Uwanja wa Hure mjini Butare nchini Rwanda.
  Mabao ya Tanzania yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 10 kwa penalti, Ally Msengi dakika ya 40 na Kelvin John dakika ya 67, wakati ya Sudan Kusini yamefungwa na Dani Thon dakika ya 25, Joseph Manase dakika ya 53 na Rehan Malong dakika 66 kwa penalti.
  Kutokana na mechi ya kwanza kumalizia kwa sare ya 0-0 Dar es Salaam, Tanzania inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini na sasa itakutana na Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAITOA SUDAN KUSINI KWA MABAO YA UGENINI AFCON U23 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top