• HABARI MPYA

  Saturday, September 17, 2022

  MAYELE APIGA TENA HAT-TRICK YANGA YAUA 5-0 AFRIKA


  YANGA SC imefanikiwa kwenda Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 5-0 leo dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na kiungo Farid Mussa Malik dakika ya 47 na washambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 58 na Mkongo Fiston Kalala Mayele leo tena amefunga mabao matatu dakika za 60, 63 na 66.
  Yanga inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 9-0 baada ya kuichapa Zalan 4-0 kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita hapo hapo Mkapa, siku ambayo pia Mayele alipiga hat-trick, bao lingine akifunga kiungo Mzanzibari, Feisal Salum.
  Yanga sasa itakutana na mshindi wa jumla kati ya St George ya Ethiopia na Al Hilal Omdurman ya Sudan. Mechi ya kwanza, St. George ilishinda 2-1 nyumbani na kesho watakuwa ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA TENA HAT-TRICK YANGA YAUA 5-0 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top