• HABARI MPYA

  Sunday, September 11, 2022

  LUSAJO AING’ARISHA NAMUNGO FC MAJALIWA, YAILAZA RUVU 1-0

  BAO la Relliant Lusajo dakika ya 82 limeipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Ushindi huo unaifanya Namungo FC ifikishe pointi saba baada ya mechi tatu, mbili za awali ikishinda moja na sare moja.
  Kwa Ruvu Shooting baada ya kuchapwa leo, wanabaki na pointi zao tatu za mechi tatu pia, leo wakipoteza mechi ya pili baada ya awali kushinda moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUSAJO AING’ARISHA NAMUNGO FC MAJALIWA, YAILAZA RUVU 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top