• HABARI MPYA

  Monday, September 26, 2022

  TWAHA KIDUKU AMTWANGA BONDIA WA MISRI MTWARA

  BONDIA Twaha Kassim Rubaha juzi usiku alimshinda Abdo Khalid wa Misri Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kutetea ubingwa wa UBO Afrika huku akiongeza taji la Mabara la UBO. 

  Kulikuwa kuna mapambano mengine kadhaa ya utangulizi, likiwemo la bondia 'kichekesho' Karim Mandonga wa Morogoro ambaye kama kawaida lichapwa kwa Knockout (KO) na Salim Abeid wa Tanga. Naye Adam Lazaro alimshinda kwa pointi mkongwe Francis Miyeyusho katika pambano lingine tamu la utangulizi usiku huo. Mtoto wa nyumbani, Mtwara Osama Arabi 'akafundishwa' ndondi na mkongwe wa Emmilian Patrick wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika pambano lililovutia wengi. Joseph Mchapeni akamchapa Paschal Goba kwa pointi katika pambano lingine lililoteka hisia za wengi usiku huo Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWAHA KIDUKU AMTWANGA BONDIA WA MISRI MTWARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top