• HABARI MPYA

  Wednesday, September 07, 2022

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA IHEFU 3-1 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 45, Issa Rashid dakika ya 50 na Nickson Kibabage dakika ya 82, wakati la Ihefu limefungwa na Andrew Simchimba dakika ya nane.
  Ihefu ilipoteza nafasi ya kupata bao baada ya mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa kukosa penalti dakika ya 85 baada ya Juma Nyangi kumuangusha Issa Ngoah kwenye boksi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA IHEFU 3-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top