• HABARI MPYA

  Sunday, September 11, 2022

  GEITA GOLD YACHAPWA 1-0 NA AL HILAL SUDAN


  TIMU ya Geita Gold imechapwa 1-0 na wenyeji, Al Hilal Port Sudan katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman.
  Bao pekee la Al Hilal limefungwa na Omer Shamali dakika ya tano na timu hizo zitarudiana Septemba 17 Uwanja Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mshindi wa jumla atamenyana na Pyramids ya Misri katika Raundi ya Pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YACHAPWA 1-0 NA AL HILAL SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top