// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IBRAH CLASS YUKO TAYARI KUMCHAKAZA MMEXICO KESHO MLIMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IBRAH CLASS YUKO TAYARI KUMCHAKAZA MMEXICO KESHO MLIMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, September 29, 2022

    IBRAH CLASS YUKO TAYARI KUMCHAKAZA MMEXICO KESHO MLIMANI


    BONDIA wa Tanzania Ibrahim Class anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mpinzani wake kutoka Mexico, Gustavo Pina katika pambano la kimataifa la uzito wa feather litakalofanyika kesho (Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City.
    Akizungumza mara baada ya kupima uzito jana, Pina alisema kuwa kamwe hawzi kupoteza mapmbana mawili mfululizo na amekuja ili kurekebisha rekodi yake baada ya kupoteza pambano la ubingwa wa WBA dhidi ya bondia kutoka Panama, Anselmo Moreno mwezi Machi mwaka huu.
    Alisema kuwa anajua anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Class, lakini amejiandaa vilivyo kwai hawezi kurejea makosa yake tena. Kwa mujibu wa rekodi, Class ameshinda mapambano 27 ambapo kati ya hayo, 12 kwa njia ya KO na kupoteza mapambano sita ambapo mawili kwa njia ya KO.
    Pina ameshinda mapambano 10, matano kwa KO na kupoteza mawili yote kwa KO.
    “Nimesafiri umbali mrefu kuja hapa Tanzania si kwa kushindwa, lengo kuu ni kushinda, hivyo Class ajiandae kwani siwezi kupoteza kamwe,” alisema Class.
    Kwa upande wake, Class alisema kuwa pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Pina, lengo lake la ushindi na kuwaomba Watanzania kufika kwa wingi.
    “Ushindi wangu wa KO upo pale pale na si vinginevyo. Nimejiandaa vyema kwa ajili ya kuwapa heshima Watanzania na si  vinginevyo,” alisema Class. 
    Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya MO Boxing, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo chini ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji.
    Mratibu wa pambano hilo kutoka MO Promotion Ahmed Seddiqi alisema kuwa maandalizi yamekamilika na ambapo kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi.
    Pambano la kwanza la utangulizi litakuwa kati ya bondia nyota wa Ghana, Alfred Lamptey ambaye atapambana na bondia Abraham Ndauendapo kutoka Namibia huku Juma Choki akizichapa na bondia wa kutoka Mexico Jose Hernandez ambapo bondia kutoka Kenya Nicholas Mwangi atapimana ubavu na Emmanuel Mwakyembe wa Tanzania.
    Pambano lingine litakuwa baina ya bondia Sameer Anwar dhidi ya Adam Mrisho huku Mwinyi Mzengelaakizichapana Sabari J na pambano lingine litakuwa baina ya Lulu Kayage dhidi ya Sadra Mohamed.
     Pambano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Azam TV, Boxer, MO XTRA, Mlimani City, KCB Bank, White Sands Resorts, Bajaj na OTAPP.


    Mabondia wa kike Lulu Kayage (kulia) na Sadra Mohamed wakitambiana kabla ya pambano lao la kesho.
     
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IBRAH CLASS YUKO TAYARI KUMCHAKAZA MMEXICO KESHO MLIMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top