• HABARI MPYA

  Saturday, September 10, 2022

  PHIRI APIGA BONGE LA BAO SIMBA YAWACHAPA WAMALAWI 2-0 KWAO


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Nyasa Big Bullets katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.
  Mabao ya Simba SC ambayo leo iliongozwa na kocha wa 'kukodishwa' kutoka kwa wapinzani wa Ligi Kuu ya nyumbani, Coastal Union, Juma Mgunda yamefungwa na washambuliaji Mzambia, Moses Phiri kwa tik tak dakika ya 29 na mzawa, John Bocco dakika ya 84.
  Timu hizo zitarudiana Septemba 18 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya kati ya Red Arrows ya Zambia na Primiero do Agosto ya Angola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI APIGA BONGE LA BAO SIMBA YAWACHAPA WAMALAWI 2-0 KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top