• HABARI MPYA

  Sunday, September 18, 2022

  YANGA NA AL- HILAL, SIMBA NA AGOSTO


  WAPINZANI wapya wa Yanga SC katika Raundi ya mwisho ya kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni Al-Hilal FC ya Omdurman nchini Sudan.
  Hiyo ni baada ya Al-Hilal kuitoa St George ya Ethiopia kwa faida ya bao la ugenini kufuatia sare ya jumla y 2-2.
  Mechi ya kwanza mjini Addis Ababa, St. George ilishinda 2-1, kabla ya leo kuchapwa 1-0 mjini Omdurman, hivyo Al Hilal wanasonga mbele kwa faida ya bao walilopata Ethiopia. 
  Timu nyingine ya Tanzania, Simba yenyewe itamenyana na Primiero do Agosto ya Angola katika Raundi ya mwisho wa kuwania kucheza Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Kwa upande wao, Primiero de Agosto ya Angola imefika Hatua hii kwa kuitoa Red Arrows ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 ugenini wiki iliyopita na sare ya 1-1 nyumbani leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA AL- HILAL, SIMBA NA AGOSTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top