• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2022

  HAALAND APIGA BONGE LA BAO DHIDI YA TIMU YAKE YA ZAMANI


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Man City yamefungwa na John Stones dakika ya 80 na Erling Haaland dakika ya 84 kwa tik-tak, wakati la Borussia Dortmund limefungwa na Jude Bellingham dakika ya 56.
  Ushindi huo wa pili unaifanya Man City ifikishe pointi sita na kuendelea kuongoza kundi kwa pointi tatu zaidi ya Dortmund baada ya wote kucheza mechi mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA BONGE LA BAO DHIDI YA TIMU YAKE YA ZAMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top