• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2022

  POTTER AANZA NA SARE CHELSEA


  KOCHA mpya, Graham Potter ameanza sare ya 1-1 Chelsea dhidi ya RB Salzburg usiku wa Jumatano katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Chelsea walitangulia na bao la Raheem Sterling dakika ya 48, kabla ya Noah Okafor kuisawazishia RB Salzburg dakika ya 75.
  Chelsea inaendelea kushika mkia Kundi E kwa pointi yake moja nyuma ya RB Salzburg yenye pointi mbili, Dinamo Zagreb pointi tatu na AC Milan pointi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POTTER AANZA NA SARE CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top