• HABARI MPYA

  Wednesday, September 28, 2022

  ALLY KAMWE AFISA HABARI MPYA YANGA SC


  MCHAMBUZI na Mwandishi wa Habari wa Azam Tv, Ally Kamwe ameteuliwa kuwa Afisa Habari wa klabu ya Yanga, nafasi iliyoachwa wazi na Hassan Bumbuli aliyemaliza muda wake.


  Aidha, Mwandishi mwingine wa Habari, Priva Abiud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mitandao ya Kijamii ya klabu hiyo.
  Kwa upande wake, CPA Haji Mfikirwa - amehamishwa idara na kuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki ( Members and Fans Engagement).


  CPA Mfikirwa ni msomi mwenye shahada ya biashara na mbobezi wa fani ya uhasibu, alijiunga na Klabu ya Yanga tangu Mwaka 2020 na amefanikisha maboresho makubwa katika idara ya Fedha na utawala wa Klabu. 
  Kutokana na utendaji wake mzuri na mafanikio aliyoyapata katika idara ya fedha, uongozi wa juu wa Klabu umeamua kumhamishia kwenye idara hii mpya ambayo ni mhimili Mkubwa katika muundo huu mpya wa uendeshaji wa Klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLY KAMWE AFISA HABARI MPYA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top