• HABARI MPYA

  Sunday, September 04, 2022

  MANCHESTER UNITED YAIZIMA ARSENAL, YAICHAPA 3-1 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wamezima wimbi la ushindi la Arsenal katika mchezo wa sita baada ya kuitandika mabao 3-1 leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mshambuliaji mpya kutoka Ajax, Mbrazil, Antony Matheus dos Santos aliifungia bao la kwanza Man United dakika y 35 akimalizia pasi ya mshambuliaji Muingereza, Marcus Rashford ambaye alifunga mabao mengine mawili dakika ya 66 akimalizia pasi ya Bruno Fernandes na 75 akimalizia kazi nzuri ya C Eriksen.
  Bao pekee la Arsenal katika mchezo huo limefungwa na mshambuliaji Muingereza, Bukayo Saka dakika ya 60, The Gunners wakipoteza pointi kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kushinda mechi tano mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YAIZIMA ARSENAL, YAICHAPA 3-1 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top