• HABARI MPYA

  Friday, September 16, 2022

  RONALDO AFUNGA MAN UNITED YASHINDA 2-0 UGENINI ULAYA


  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji, FK Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi E michuano ya UEFA Europa League jana Uwanja wa Stadionul Zimbru mjini Chisinau.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Sancho dakika ya 17 na Cristiano Ronaldo kwa penalti dakika ya 39, huo ukiwa ushindi huo kwanza na sasa wanazidiwa pointi tatu na vinara, Real Sociedad baada ya wote kucheza mechi mbili.
  Kwa upande wao, Sheriff wana pointi tatu pia, huku Omonia Nicosia ambayo haina pointi inashika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA MAN UNITED YASHINDA 2-0 UGENINI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top