• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2022

  REAL MADRID YAICHAPA RB LEIPZIG 2-0 BERNABEU


  MABAO ya Fede Valverde dakika ya 80 na Marco Asensio dakika ya 90 na ushei yameipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya RB Leipzig katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Real Madrid inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi F mbele ya Shakhtar Donetsk yenye pointi nne na Celtic pointi moja, wakati RB Leipzig inashika mkia ikiwa haina pointi baada ya wote kucheza mechi mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA RB LEIPZIG 2-0 BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top