• HABARI MPYA

  Wednesday, September 14, 2022

  MKUDE AIBEBESHA SIMBA POINTI TATU MBELE YA PRISONS MBEYA


  BAO pekee la kiungo Jonas Mkude dakika ya 86 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya ushindi huo na kuungana kileleni na mabingwa watetezi, Yanga kwa kulingana hadi wastani wa mabao baada ya wote kucheza mechi nne.
  Tanzania Prisons yenyewe inabaki na pointi zake nne za mechi nne pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKUDE AIBEBESHA SIMBA POINTI TATU MBELE YA PRISONS MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top