• HABARI MPYA

  Tuesday, September 06, 2022

  GEITA GOLD NA KAGERA SUGAR ZATOA SARE, 1-1 KIRUMBA


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Kagera Sugar walitangulia na bao Abeid Athumani dakika ya 44, kabla ya Suleiman Ibrahim kuisawazishia Geita Gold dakika ya 74.
  Ni sare ya pili kwa Geita Gold baada ya awali kupoteza mechi moja mbele ya Simba wako napas 3-0 na kutoa droo na Azam FC mechi zote zikipigwa Dar es Salaam.
  Kwa Kagera Sugar ni sare ya kwanza baada ya kupoteza mechi zote za awali ugenini mbele ya Simba na Azam FC Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD NA KAGERA SUGAR ZATOA SARE, 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top