• HABARI MPYA

  Tuesday, September 20, 2022

  SSEMWOGERERE KOCHA MPYA PAMBA FC


  NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, George Ssemwogerere ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Pamba ya Mwanza akichukua nafasi ya Mkenya, Yussuf Chipo aliyehamia Coastal Union ya Tanga.
  Pamba, mabingwa wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapambana kurejea Ligi Kuu kutoka Championship iliyoanza mwishoni mwa wiki wakipata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Ken Gold ya Mbeya.
  Mechi hiyo ya kwanza timu ilikuwa chini ya kocha mwingine mzoefu nchini, Steven Matata aliyekuwa Msaidizi wa Chipo wakati wa maandalizi ya msimu na mechi ijayo Jumamosi dhidi ya Mbeya Kwanza ndiyo Ssemwogerere ataanza kazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SSEMWOGERERE KOCHA MPYA PAMBA FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top