• HABARI MPYA

  Thursday, September 29, 2022

  OKRAH APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KIPANGA 3-0


  KLABU ya Simba imekamilisha ziara yake ya mechi za kirafiki visiwani Zanzibar kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Kipanga usiku wa Jumatano Uwanja wa Amani.
  Mabao ya Simba yamefungwa na viungo washambuliaji Mghana, Augustine Okrah mawili, dakika ya 36 na 59 na Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis dakika ya 65.
  Huo ni ushindi wa pili kwenye ziara yao hiyo ya wiki moja kipindi hiki cha mapumziko mafupi ya Ligi Kuu ya Bara, baada ya awali kuichapa Malindi 1-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKRAH APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KIPANGA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top