• HABARI MPYA

  Wednesday, September 21, 2022

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SINGIDA STARS 1-1 KIRUMBA


  TIMU ya Geita Gold imelazimishwa sare ya 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Geita Gold ilitangulia na bao la mfungaji bora wa msimu uliopita, George Mpole dakika ya tisa tu, kabla ya Mbrazil Rodrigo Figueiredo kuisawazishia Singida Big Stars dakika ya 42:
  Kwa matokeo hayo, Singida Big Stars inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya tano, wakati Geita Gold sasa wana pointi tatu katika nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SINGIDA STARS 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top